Blog ya mzungu

Mimi ndio mzungu, na nataka nitupe maneno yangu hapa. So ukipenda unaweza kuyasoma!

Thursday, October 06, 2005

Kurudi shuleni II

Baada ya kupumzika siku moja (ilikuwa kazi sana, kwenda shule dakika tano...), leo ilikuwa siku la pili.
Bahati nzuri, mwalimu alikuwepo. Somo hilo ni ya 'minor' yangu. Jina la somo ni 'Gender & Diversity' (jinsia na kutofautiana). Jina la minor ni Ukuwaji, Siasa na Maendelezo.
Walikuwa wanafunzi wengi darasani, kama mia moja. Wote wa faculty yangu wanaweza kufuata somo hilo, sio wanafunzi wa masomo ya kiafrika tu. Lakini sisi wa 'kiafrika' tulikuwepo karibu na wote.
Nimefikiri somo lilivutia. Lakini nimeshasoma kidogo kuhusu jinsia, kwa hivyo ilikuwa habari ya zamani. Lakini bado nimelipenda.
Nimeshangaa kwamba hapa wanafunzi wameendelea kuongea, hata wakati mwalimu alifundisha. Kwetu ni lazima tuwe kimya, au mwalimu atatutupa nje. Na pia amesema ile Bachelor ni mpya halafu tunatarajiwa kusoma wenyewe, inakubidi usome kitabu na ufutilie kila neno kwa ufasaha badala ya kutoa kichwani mwako. Sasa, vitu vya bachelor ni vya kawaida kwetu. Kabla hatujaanza kusoma shahada ya pili hatu hitaji kurudia tuliyosoma ingawa tunahitaji kujifikiria.

Kurudi shuleni

Hatimaye, shule imeanza. Lakini hobela sijafuata masomo. Nimesubiri miezi minne na jumanne ingekuwa siku la kwanza, somo la Ciluba (lugha ya Kongo). Nilichelewa kidogo na nimeona mwalimu mwingine. Nimeenda kukaa darasani na nimemsikiliza mwalimu huyu.
Alipomaliza hadithi yake kuhusu minor tunalazimishwa kuchagua, ametuambia mwalimu Kabuta wa Ciluba hataweza kutufundisha ile siku..
Ilikuwa mwisho wa somo, na tumerudi wote nyumbani..

Saturday, August 20, 2005

Ujamaa

Nimemaliza makala yangu kuhusu Ujamaa na RDA :) Labda sasa naweza kupata Propedeuse yangu, maanake nimeshinda masomo yote ya mwaka la kwanza shuleni. Halafu naweza kuwaambia watu nimesoma kweli haha. Lakini siwezi kusema najua nini sasa, ok, naongea kiswahili kidogo, lkn zaidi.. sijui. Sijamaliza. Nitasoma hapa Gent pia miaka miwili. Na nimeelewa sasa tofauti kabisa. Watu walishtuka kusikia nimechelewa kumaliza makala kuliko mwaka moja. Sijui itakuwaje hapa. Huwezi kuendelea mpaka umeshinda kila somo! Bahati nzuri nitaishi pamoja na wawili wanaosoma pamoja na mimi, na pia rafiki yangu wa Brazil atakaa hapa Gent, nimefurahi sana :)
Nimefurahi nimepata marafiki mengi wanaoongea Kiswahili hapa, sitasahau lugha. Pia nimekutana na mbelgium mmoja ana mpenzi wa Rwanda, na sasa anataka kusoma Kiswahili pia, mimi tamsaidia kidogo na pia niko na rafiki wa kizungu :) haha
ok poa basi hii ni za kutosha 4 2day!

Friday, August 19, 2005

Karibuni!!

Nimerudi, haha. Nishaanza kuandika masiku mengi yaliyopita, lkn sikuendelea sana. Lakini nipo tena, na nitajaribu kujisikisha (?) mara kwa mara. Sina mengi la kusema, au, ninalo, lkn nina kazi ya kufanya.
Nikimaliza nitarudi nanyi. Nawapa ninyi hi tu!